MAWAZIRI KADHAA WAKABIDHIWA AFISI

Aliyekuwa Waziri wa hazina ya kitaifa Njuguna Ndung’u ameondoka rasmi afisini na kumkabidhi mrithi wake John Mbadi wakati wa hafla fupi ambako Waziri Mbadi ameahidi kuendeleza mikakati ya kuimarisha uchumi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Profesa Ndung’u ameelezea aliyofanikisha katika muda wa miaka 2 alipokuwa Waziri, ikiwemo kuweka mikakati ya kuondoa wafanyakazi hewa katika sekta ya umma.
Wakati uo huo, Waziri wa mazingira Aden Duale amechukua rasmi usukani kutoka kwa mtangulizi wake Soipan Tuya ambaye naye amemrithi Duale katika wizara ya ulinzi.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa