MRADI WA UMEME WAZINDULIWA BUNGOMA

Shughuli za masomo, viwanda na usalama katika kaunti ya Bungoma zimepigwa jeki baada ya kaunti hiyo kuzindua mradi wa usambazaji umeme katika kaunti zote 45, utakaogharimu shilingi milioni 90. Mradi huo unaendeshwa na serikali ya kaunti ya Bungoma kwa ushirikiano na shirika la REREC, gavana Ken Lusaka akielelezea matumaini ya kuboreshwa kwa Maisha ya wakazi […]

JAMII YATAKIWA KUKOMESHA DHULUMA ZA KIJINSIA

Dhuluma za kijinsia zimeendelea kuwa donda sugu ulimwenguni kote huku wito ukitolewa kwa jamii katika siku 16 za kampeni ya kukomesha dhuluma hizo. Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa UN, wanawake na wasichana 140 huuawa kila siku na wapenzi au watu walio karibu nao. Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo, wanaharakati nchini […]

TAASISI YA SILICON SAVANA YAZINDULIWA KUIMARISHA UHANDISI

Sekta ya uhandisi nchini imepigwa jeki baada ya Rais William Ruto kuzindua ujenzi wa taasisi ya kisasa ya uhandisi maarufu kama Silicon Savanah kuwezesha utafiti na uvumbuzi. Ujenzi huo utaotekelezwa katika kipindi cha miaka 5 kwa gharama ya shilingi bilioni 3, utafanywa katika chuo kikuu cha Nairobi, ukifadhiliwa na serikali ya Ufaransa. Akizungumza wakati wa […]

‘WAKONGWE’ WA MOI WASHINIKIZA NAIBU CHANSELA AONDOKE

Serikali imetakiwa kumtimua msimamizi wa chuo kikuu cha Moi Profesa Isaac Kosgey na kuvunjilia mbali baraza la chuo hicho ili kuwawezesha wanafunzi chuoni humo kurejelea masomo na kuyakamilisha kwa wakati. Wakizungumza na wanahabari, wanafunzi wa zamani wa chuo hicho wamelalamikia mgomo wa wahadhiri ambao umeendelea kwa miezi kadhaa, na kuwaonya wanasiasa dhidi ya kuingilia usimamizi […]

KILIO CHA WAKULIMA WA KAHAWA BUNGOMA

Uuzaji haramu wa zao la kahawa katika kaunti ya Bungoma kwa mawakala nchini Uganda ndicho chanzo cha kudorora kwa vyama vya ushirika vya kahawa kwenye kaunti hiyo. Haya ni kwa mujibu wa afisa wa vyama vya ushirika katika eneo bunge la Mlima Elgon Eric Kibet, ambaye ameapa kuweka masharti makali miongoni mwa kamati za vyama […]

WIZARA YA VIJANA YAZINDUA KAMATI YA JINSIA NA UTEKELEZAJI LEO

Wizara ya masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo inapanga kuzindua kamati ya masuala ya jinsia na utekelezaji hii leo. Hafla hiyo itaongozwa na waziri wa masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo Kipchumba Murkomen, na inapangiwa kuandaliwa katika jumba la Talanta Hela muda wowote kuanzia sasa. Kamati hiyo imejukumiwa kuimarisha usawa wa […]

MATUMAINI YA KNUT YA KUFIKIA MAKUBALIANO NA TSC

Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu (KNUT), Collins Oyuu, amewahakikishia walimu kuwa mazungumzo yao na Tume ya Huduma za Walimu (TSC) kuhusu Mkataba wa Pamoja wa Makubaliano (CBA) yanaendelea vizuri. Oyuu, akizungumza mjini Rongo, Kaunti ya Migori, amesema maafisa wa chama wamekuwa na mikutano kadhaa na TSC. Akieleza matumaini kwamba mahitaji ya walimu […]

GAVANA WAIGURU APENDEKEZA KUBUNIWA KWA KITENGO MAALUM CHA KUKABILI MAUAJI YA WANAWAKE

Huku taifa la Kenya likisherehekea siku 16 za uhamasishaji kuhusu jinsia, Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru, amezitaka mamlaka kuunda kitengo maalum cha polisi ndani ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) ili kushughulikia ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake nchini. Waiguru amesema kitengo hiki ndani ya muundo wa DCI kitasaidia kuchunguza na kuzuia mauaji […]

KIJANA AJINYONGA CHERANGANI, POLISI WAANZA UCHUNGUZI

Maafisa wa polisi wameanzish uchunguzi kuhusiana na kisa cha Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 28 ambaye amejitoa uhai kwa kujinyonga katika eneo la Chepsiro Cherangani kaunti ya Transnzoia kufuatia kile kinakisiwa kuwa msongo wa mawazo usiku wa kuamkia leo. Kulingana na chifu wa eneo hilo Gilbert Chepsiror mwendazake Aliakima Kipruto alikuwa mraibu wa pombe […]

LEICESTER YAMFUTA KAZI MENEJA STEVE COOPER

Leicester ilimfuta kazi meneja Steve Cooper, huku timu hiyo ikiwa na alama mbili tu juu ya eneo la kushushwa daraja katika Ligi Kuu ya Uingereza. Cooper, mwenye umri wa miaka 44, hakuwa chaguo maarufu alipoajiriwa kuchukua nafasi ya Enzo Maresca mwezi Juni kutokana na historia yake na wapinzani wa karibu, Nottingham Forest. Aliweza kushinda mechi […]