SHULE YA MUMBUNI MACHAKOS YAFUNGWA

Shule ya upili ya wavulana ya Mumbuni kwenye kaunti ya Machakos imefungwa kwa mda usiojulikana baada ya mali ya thamani isiyojulikana kuteketea kwenye moto uliochoma sehemu ya bweni, lenye wanafunzi 220 wa kidato cha pili na kidato cha tatu usiku wa kuamkia leo.
Kwa sasa hakuna majeruhi wameripotiwa pale shuleni na wazazi wapo katika lango kuu kuwachukua watoto wao
Kulingana na afisa wa maswala ya kudhibiti moto kwenye kaunti ya Machakos, Francis Nzioki, chanzo cha moto hakijabainishwa hadi wa sasa. Moto huo ulianza usiku baada ya wanafunzi kurejea kwenye mabweni baada ya masomo ya ziada ya jioni.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi katika kaunti ya Machakos, Patrick Lobolia, maafisa wa polisi tayari wamewakamata wanafunzi sita wanaohusishwa na kisa cha mkasa huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa