#uncategorized

IDADI YA VIFO KUTOKANA NA MAFURIKO NI 299, KITHURE ASEMA

Waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki amesema kuwa jumla ya watu 299 wamefariki kutokana na mafuriko hapa nchini, 75 wasijulikane waliko huku wengine 188 wakiuguza majeraha.

Kulingana na Kindiki, mafuriko hayo yamewaathiri familia 55,631, huku jumla ya watu 278,155 wameathirika.

Aidha, kambi 187 zimewekwa katika kaunti 25 kote nchini kuwapa hifadhi waathiriwa, kaunti ya Busia ikiwa miongoni mwa kaunti zilizoathirika pakubwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *