DCI WACHUNGUZA MAUAJI YA NANCY WANJOGU NYERI
Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wanachunguza mauaji ya Nancy Wanjogu mwanamke mwenye umri wa miaka 26 ambaye mwili wake umepatikana katika nyumba yake kijiji cha Kwamuya,Karatina, Kaunti ya Nyeri.
Kulingana na Polisi mwili huo ulikuwa na majeraha mabaya wakati ulipogunduliwa ,kakake marehemu amewaambia polisi kwamba alipokea simu kutoka kwa marehemu kwamba maisha yake yalikuwa hatarini na kuchukua hatua ya kufululiza moja kwa moja hadi katika chumba cha dadaye na alipofika eneo la tukio akapata maiti ya dadaye ikiwa imelala chini huku damu zikiwa zimetapakaa pembeni yake.
Mwili huo umepelekwa katika Hospitali ya Karatina Level IV ukisubiri uchunguzi
Mshukiwa ametambuliwa na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Imetayrishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































