POLISI AUAWA NAKURU, WENZAKE WAJERUHIWA
Afisa mmoja wa polisi ameuawa kwa risasi huku wenzake 2 wakijeruhiwa na watu wanaoaminika kuwa magenge ya wahalifu wakati polisi walipokuwa wakishika doria katika eneo la Free Area jijini Nakuru usiku wa kuamkia leo.
Waliojeruhiwa ambao ni maafisa wa kituo cha polisi cha Bondeni, wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nakuru level 5.
Kamishna wa kaunti ya Nakuru Loyford Kibaara, amesema tayari washukiwa kadhaa wamekamatwa wakiwa na bunduki aina ya AK-47.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































