MASAIBU YA MOI YAKOSA KIKOMO

Huenda shughuli za masomo zikakosa kurejelewa katika chuo kikuu cha Moi baada ya wahadhiri wa chuo hicho kuapa kuendelea na mgomo wao ambao umedumu kwa miezi 3, licha ya chuo hicho kuwataka wanafunzi warejee wiki ijayo.
Kwa mujibu wa wahadhiri hao, watarejea kazini tu iwapo wizara ya elimu itakubali ombi lao la kutaka usimamizi mpya chuoni humo, mbali na kulipwa kwa mishahara yao kikamilifu.
Aidha, wamesema kuwa masaibu ya chuo hicho ikiwemo madeni ya takribani shilingi bilioni 9 yanmesababishwa na usimamizi mbaya na utumizi mbaya wa fedha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa