UCHAGUZI WA FKF WAPANGWA TAREHE SABA DISEMBA

Bodi ya Uchaguzi ya FKF imepanga tarehe 7 Disemba kuwa tarehe ambayo kura za urais zitafanyika katika kile ambacho kitakuwa kilele cha mchakato ambao umekuwa na panda shuka nyingi kwa miezi kadhaa.
Kwa mujibu taratibu za kuelekea uchuaguzi huo iliyotolewa na Bodi hiyo ya Uchaguzi hii leo, Kamati ya Utendaji ya kitaifa na wawaniaji urais wamepangwa kuwasilisha majina yao Oktoba 14 watakapojulikana wale wote wanaowania nafasi hiyo.
Orodha ya mwisho ya wagombeaji waliohitimu kitaifa na kaunti itachapishwa mnamo Novemba 2.
Uchaguzi wa urais utatanguliwa na kura za Kaunti zitakazofanyika Novemba 9.
Orodha ya mwisho ya Wajumbe 94 wa Uchaguzi wa Kitaifa itachapishwa Novemba 23, wiki mbili kabla ya kura za urais.
Imetayarishwa na Nelson Andati