AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIAMBU

Maafisa wa upelelezi wanachunguza kisa ambapo mwanamume mmoja amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana katika eneo la Kist, mji wa Kiambu.
Polisi wamefika eneo la tukio na kukuta maiti ya mtu asiyejulikana mwenye umri wa takriban miaka 27 ikiwa imelala kando ya pikipiki.
Mwili huo ulikuwa na jeraha moja la risasi kifuani huku cartridge na risasi moja ikipatikana takriban mita 100 kutoka ulikokuwa mwili huo.
inadaiwa kuwa mwendesha pikipiki huyo alikuwa akifuatwa na waendesha pikipiki wengine wawili ambao walikimbia eneo la tukio mara baada ya kupigwa risasi.
Mwili huo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City ukisubiri uchunguzi wa maiti na kutambuliwa.
Imetayarishwa na Janice Marete