WAUGUZI WATOA ILANI YA MGOMO

Muungano wa wauguzi nchini umetoa makataa ya siku 21 kwa serikali kutoa kima cha shilingi bilioni 11 kwa serikali za kaunti ili kufanikisha zoezi la kuwaajiri wauguzi Zaidi la sivyo uitishe mgomo wa kitaifa na kulemaza matibabu. Katika kikao na wanahabari jijini Mombasa, katibu mkuu wa muungano huo Seth Panyako amelalamikia jinsi mgao huo umecheleweshwa […]

MADAKTARI KUTRH WAGOMA, WATATIZA MATIBABU

Shughuli za matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya chuo kikuu cha Kenyatta zimesambaratika kufuatia mgomo wa madaktari hospitalini humo ambao umeanza hii leo. Madaktari hao wanalalamikia kusitishwa kwa bima ya afya na kile wanachokitaja kuwa usimamizi mbaya wa hospitali hiyo, na kutishia kusitisha huduma zote iwapo malalamishi yao hayataangaziwa. Kulingana nao, kaimu afisa […]

RAIS RUTO ATETEA BIMA YA AFYA SHA, AHIMIZA WANANCHI KUJISAJILI

Kwa mara nyingine Rais wiliam Ruto amejitokeza kutetea bima ya afya SHA akisisitiza manufaa yake kwa wananchi Kwa mujibu wa Ruto SHA inawajali wakenya walio na mapato ya chini au bila mapato yoyote vile vile kukabiliana na mapungufu ambayo yamekuwa yakiwakumbna wananchi chini ya bima ya afya ya awali NHIF. Ruto aidha am ewahimiza wakenya […]

KENYA YAADHIMISHA MIAKA 60 YA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA NAIROBI

Sherehe za kuathimisha miaka 60 ya kidiplomasia zinaendelea jijini Nairobi huku mkuu wa mawairi Musalia Mudavadi akiongoza sherehe hizo. Wakenya ambao wamechangia pakubwa katika shughuli za kidiplomasia wamepata fursa ya kupokeatuzo kwenye hafla hiyo. Wanariatha mabigwa akiwemo Faith Kipyegon, Eliud Kipsonge wamepokezwa tuzo hizo huku timu ya kitaifa ya mchezo wa raga na shirika la […]

AMORIM APATA USHINDI WA KWANZA KATIKA LIGI KUU, CHELSEA WAPANDA TATU

Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, alipata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuishinda Everton 4-0, huku Manchester City inayokabiliwa na changamoto ikijaribu kufufua matumaini yao ya kutwaa taji katika mechi kali dhidi ya vinara wa ligi, Liverpool. City, ambao wanashika nafasi ya tano, walianza mechi yao Anfield wakiwa katika […]

SHAHADA YA KIFO JUU YA MAPENZI

Maafisa wa usalama wameanisha uchuguzi kufuatia kifo cha mwanafunzi wa chuo cha utabibu mnjini kitale ambaye alitarajiwa kufuzu siku ya alhamisi wiki hii. Marehemu Benedict Kiptoo anadaiwa kuuliwa na mpenziwe kwa kudungwa kisu kufuatia mzozo wa kimapenzi. Kulingana na naibu kamanda wa kaunti ya Transnzoia Salesia Murithi marehemu ameuliwa na mpenziwe na kwamba wanaendeleza msako […]

MOMBASA UNITED WATOKA SARE YA 1-1.3K FC

Timu ya 3K FC kutoka Embu ililazimishwa sare ya 1-1 na Mombasa United katika mechi ya Ligi Kuu ya Taifa iliyochezwa Jana alasiri kwenye Uwanja wa Serani, jijini Mombasa. Glen Githinji alifunga kwa niaba ya 3K, huku mchezaji wa zamani wa Bandari FC, Wilberforce Lugogo, akifunga bao la kusawazisha kwa Mombasa United. Akizungumza baada ya […]

KAUNTI YA MIGORI YAZINDUA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WAZEE WASIOJIWEZA

Serikali ya kaunti ya Migori imeanzisha mpango wa kusajili na kulipia bima ya afya kwa wazee wasiojiweza ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi. Afisa mkuu wa huduma za matibabu wa Kaunti ya Migori, Samwel Atula, amesema Idara ya Afya ya Kaunti hiyo inashirikiana kwa karibu na Idara ya huduma za kijamii kuwatambua wazee […]

KAUNTI YA KAKAMEGA YAPITISHA SHERIA YA KUKABILIANA NA DHULUMA ZA KIJINSIA

Mashirika yasiyo ya serikali kwenye ukanda wa magaribi ya kenya yameipongeza sewrikali ya kaunti hya kakamega kwa kuonyesha uwezo wa kuithinisha sheria ya kukomesha ukatili wa kijinsia Ili kuthibiti ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia afisa mshirikishi wa taasisi moja isiyo ya serikali amesma kuwa sheria hiyo itapunguza visa vya wahalifu kuhitilafiana na kesi […]

KAYOLE STARLETS WASHINDA BANDARI QUEENS 0-1 MOMBASA

Kayole Starlets waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Bandari Queens katika mechi yenye ushindani mkali ya Ligi ya Kitaifa ya Wanawake iliyochezwa kwenye Uwanja wa Michezo wa Serani, jana Jumapili. Bao hilo pekee lilifungwa na Esther Ngugi katika kipindi cha pili, likikomesha mfululizo mzuri wa matokeo kwa Bandari Queens kwenye ligi. Kocha […]