NANI WA KULAUMIWA KATIKA SAKATA YA MBOLEA GHUSHI?

Viongozi katika kaunti ya Transnzoia maeneo yanayokuza bidhaa ya mahindi wamesema haitoshi kwa bunge la kitaifa kumwondolea lawama Waziri wa kilimo Mithika Linturi na kuachiliwa huru maafisa wengine serikalini ambao kwa njia moja au nyingine walihusika katika Sakata ya mbolea ghushi
Viongozi hao akiwemo mwakilishi wa wadi ya Sitatunga Simon Murray wamesema sharti ukweli ubainike na maafisa fisadi kuwajibishwa kisheria.
Kadhalika baadhi ya wakulima wameonyesha kutoridhishwa na hatua ya bunge kumwondolea Waziri Linturi lawama katika Sakata nzima ya mbolea ghushi.
Wakizungumza na aviation fm wakulima hao wakiongozwa na Simon Wanjala wakulima hao wanaomba serikali yha kitaifa kuingilia kati na kuwasaidia kwani kulingana nao wanakadiria hasara kubwa.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































