#Rugby #Sports

OILERS WATINGA FAINALI YA ESS

Menengai Oilers wamefuzu kwa fainali yao ya kwanza ya Eric Shirley Shield (ESS) baada ya kushinda Kabras RFC 25-20 katika nusu fainali.

Nahodha wa Oilers, Tony Oketch, ameisifu timu yake kwa uthabiti wao, akisema wachezaji wake wameonyesha moyo mkubwa licha ya changamoto za majeraha na umri mdogo.

Oilers waliongoza kwa 20-10 kufikia mapumziko na licha ya Kabras kupunguza pengo, walishikilia ushindi kwa sasa wanajiandaa kwa fainali wakilenga kutwaa taji.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *