#Football #Sports

TAIWO AWONIYI AFANYIWA UPASUAJI WA DHARURA

Mshambulizi wa Nottingham Forest Taiwo Awoniyi amefanyiwa upasuaji wa dharura baada ya kuumia tumboni alipogongana na mlingoti wakati wa mechi dhidi ya Leicester.

Awoniyi alijaribu kuendelea kucheza baada ya matibabu ya awali, lakini jeraha lake lilithibitishwa kuwa kubwa siku iliyofuata.

Tukio hilo lilizua hasira kwa mmiliki wa klabu Evangelos Marinakis aliyemkabili kocha Nuno kwa kumwacha mchezaji uwanjani.

Forest sasa wanapigania nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, huku wakiwa wamehakikishiwa kushiriki UEFA Conference League.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *