WAWAKILISHI WADI MERU WAMKANA MWANGAZA
Baadhi ya wawakilishi wadi katika kaunti ya Meru wanamtaka gavana wa kaunti hiyo Kawira Mwangaza kuondoka kwenye afisi za kaunti hiyo hadi kesi aliyowasilisha mahakamani kupinga kutimuliwa kwake itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kaunti hiyo Patrick Mutuma, wawakilishi hao wameshikilia kwamba hawamtambui Mwangaza kuwa gavana wao.
Wakati uo huo, wawakilishi wadi hao wametilia shaka uhalali wa agizo la mahakama kumbakisha Mwangaza mamlakani licha ya kuondolewa kwake kuidhinishwa na bunge la seneti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































