UAE YATOA DOLA MILIONI 15 KWA KENYA KUSAIDIA KUKABILI HADHARI ZA MAFURIKO

Mataifa ya kiarabu UAE sasa yametoa dola milioni 15 sawa na shilingi bilioni 2 za kenya kusaidia katika kudhibiti adhari za mafuriko humu nchini.
Fedha hizo zimetolewa kufuatia agizo la rais wa UAE Sheik Mohamed bin Zayed Al Nahyan kuipa kenya pesa hizo kusaidia waadhiriwa wa mafuriko.
Kupitia mtandao wa X ubalozi wa UAE humu nchini umesema rais Mohamed bin Zayed Al Nahyan ambaye ni mwenyekiti wa shirika la kimataifa la kijamii IHAC amejitolea kuhakikiksha mataifa yanayokabiliwa na hadhari za mafuriko yanapata msaada wa kutosha.