#Local News

MASTAA WA OLIMPIKI WATUZWA FEDHA

Wanariadha waliowakilisha Kenya katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka huu ambayo yamekamilika wikendi iliyopita nchini Ufaranasa, wametuzwa leo katika dhifa iliyofanyika kwenye ikulu ndogo jijini Eldoret.

Dhifa hiyo imehudhuriwa na Rais William Ruto, naibu wake Rigathi Gachagua, spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, washikadau wa riadha na viongozi wengine.

Kila mwanariadha aliyeshinda nishani ya dhahabu ametuzwa shilingi milioni 3, mshindi wa fedha akipokezwa milioni 2, huku washindi wa shaba wakituzwa milionni moja kila mmoja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Ruto amehimiza ushirikiano baina ya serikali kuu na zile zakaunti ili kukuza talanta nchini.

Naye Waziri wa michezo Kipchumba Mukromen amewapongeza wanariadha hao kwa kufanya vyema, na kuwashutumu wakenya waliowakashifu wanariadha hao, naye nahodha wa Team Kenya Faith Kipyegon akipongeza serikali kwa usaidizi wake kwa wanariadha.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MASTAA WA OLIMPIKI WATUZWA FEDHA

VIGEZO HITAJIKA KABLA YA KUWA JIJI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *