RUTO; WAFISADI WATAONA CHA MTEMA KUNI
Wafisadi wametakiwa kuacha mara moja kujinufaisha na mali ya umma kwani kulingana na Rais william Ruto watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Ruto aidha ameahidi kuhakikisha kuna uwazi serikalini akisema kuwa yeye binafsi yuko tayari kuwajibishwa,kujukumishwa na kukosolewa.
Katika hotuba yake wakati wa kuzindua mpango wa kimkakati wa kitaifa ushirikiano na utawala bora rais.
Ruto ametangaza miongozo tisa miongoni mwao ikiwa ni utoaji wa taarifa sahihi ukusanyaji wa maoni , miongoni mwa maswala mengine huku akisisitiza kujitolea kwake katika juhudi za kukabili ufisadi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































