MURKOMEN ATETEA KUSAMBARATIKA KWA SHUGHULI
Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen ametetea hatua ya polisi kufunga barabara na kuwazuia wakenya kuendelea na shughuli zao za kila siku hapo jana, akisema hatua hiyo ililenga kuwahakikishia wakenya hao usalama wao.
Katika kikao na wanahabari, Murkomen vile vile amewasifia polisi walioshika doria hapo jana, akisema walijitolea katika kulinda mali na maisha ya raia.
Hata hivyo, idara ya polisi imeripoti kuuawa kwa watu 11, huku wakenya 63 wakiwemo maafisa 52 wakijeruhiwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































