RUTO AAGIZA UPATANISHI KWA MAHAKAMA, POLISI

Kama njia mojawapo ya kuleta upatanishi na uwiano, Rais William Ruto ametoa wito kwa idara ya mahakama na ile ya polisi kukumbatia ushirikiano kuhusiana na masuala ya kitaifa, akirejelea vuta nikuvute ambayo imeshuhudiwa baina ya idara hizo katika siku za hivi karibuni.
Kupitia taarifa, Rais Ruto amezitaka idara hizo huru kukumbatia uwiano wanapotafuta usuluhishi wa suitofahamu baina yao.
Aidha, Rais amehimiza haja ya kuheshimu sheria kama njia mojawapo ya kudumisha demokrasia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa