KAUNTI YA MOMBASA KUSUBIRI KWA MUDA ZAIDI KABLA YA KUTOZA ADA YA MAEGESHO NA TAKA KATIKA BANDARI

Serikali ya kaunti ya Mombasa huenda ikalazimika kusubiri kwa muda Zaidi kabla ya kufanikisha lengo lake la kukusanya ada ya uegeshaji na udhabiti wa taka kutoka kwenye meli na matrela ya mizigo katika bandari ya Mombasa.
Hii ni baada ya mamlaka ya kitaifa ya bahari KMA kusitisha ilani ya mamlaka ya bandari KPA kukosoa kukusanya mapato ya serikali ya Mombasa licha ya kuratibiwa kuanza kufanyika leo hii.
KMA imesitisha ilani iliyotolewa na KPA ya kukusanya ushuru huo kutoka kwa meli ikialika KPA mamlaka ya kitaifa ya mazingira NEEMA, serikali ya kaunti ya Mombasa kujadili kuhusu swala hilo ili kupata suluhu ya kudumu.
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































