AFISA WA GSU AUAWA KWA KUDUNGWA KISU KATIKA MABISHANO MJINI KISUMU

Afisa wa polisi wa kitengo cha General Service Unit (GSU) aliyeuawa jana Jumatatu katika mtaa wa mabanda wa Manyatta mjini Kisumu kwa kudungwa kisu.
Kwa mujibu wa polisi Konstebo Calvince Ouma Omondi, mwenye umri wa miaka 24 alidungwa kisu shingoni na kifuani wakati wa ugomvi na watu anaowafahamu.
Wakati wa kifo chake, alikuwa katika kambi ya Turkwel GSU katika Kaunti ya Turkana.
Afisa huyo, anayetoka Kolwa katika Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki alikuwa likizoni.
Inaarifiwa kuwa alikuwa na marafiki wakati alishambuliwa na kuuawa.
Mwili huo umepelekwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti.
Imetayrishwa na Janice Marete