FAMILIA 40,000 ZAHAMA MATHARE, NGONG “KWA HIARI”
Familia 40,000 zenye watu 100,081 zinaozishi karibu na mito katika maeneo ya Mathare na Ngong zimehama kwa hiari kutoka makazi yao, Waziri wa usalama Kithure Kindiki akisema kila aliyehama amepokea shilingi elfu 10 kutoka kwa serikali.
Katika taarifa hii leo, Kindiki amesema watu walioathirika ndio watapewa kipaumbele katika makazi ya bei nafuu yanayojengwa na serikali kote nchini.
Aidha, Waziri huyo amesema serikali itajenga ua mita 30 kutoka kwenye mito hasa katika maeneo ya miji ili kuzuia unyakuzi wa ardhi hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































