AWAMU YA PILI YA UCHAGUZI WA UDA WA VYAMA VYA MASHINANI YAANZA

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinaendesha awamu yake ya pili ya uchaguzi wa mashinani katika wadi zote 40 ndani Kaunti ya Homa Bay leo jumamosi.
Hii ni baada ya uchaguzi wa mashinani wa wajumbe wa chama kutoka kituo cha kupigia kura ambao ulifanyika katika eneo hilo tarehe 24 Aprili 2024.
Uchaguzi wa leo unalenga maafisa wa chama ambao watawakilisha wadi zote 40 katika maeneo bunge manane ya Kaunti ya Homa Bay.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































