MURKOMEN: TUNAHITAJI BILIONI 40 KWA UKARABATI
Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema wizara yake inahitaji zaidi ya shilingi bilioni 40 ili kukarabati barabara ya madaraja yaliyoharibiwa na mafuriko nchini.
Akizungumza katika eneo bunge la Keses kaunti ya Uasin Gishu, Murkomen amesema uchunguzi wa awali wa mashirika mbali mbali umebaini uharibifu mkubwa, na kwamba wizara yake ina madeni ya takribani shilingi bilioni 165 ambayo hayajalipwa.
Kulingana naye, ukusanyaji wa ushuru kwa ajali ya ukarabati wa barabara umepungua kwa shilingi bilioni 11 mwaka huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































