IEBC MPYA KUNGOJA ZAIDI KUTOKANA NA KESI

Uteuzi wa kamati ya kuwateua makamishna wapya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC utakawia baada ya kesi mpya kuwasilishwa mahakamani ikipinga uamuzi wa jopo la kutatua migogoro ya kisiasa kumtangaza Augustus Kyalo Muli kuwa mwakilishi wa vyama vidogo vidogo katika kamati hiyo.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na Koki Muli, itatajwa Alhamisi wiki hii mbele ya jaji Janet Mulwa, huku mshtakiwa Augustus Muli akitangaza kwamba ataviongozo vyama 15 kugura muungano wa Azimio.
Wakati uo huo, mlalamishi anasema kwamba jopo hilo halina mamlaka kisheria, na kwamba halikumpa fursa ya kusikilizwa.
Hata hivyo, spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula ametoa wito kuharakishwa kwa kubuniwa kwa jopo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa