#uncategorized

WATOTO WAKO KATIKA HATARI YA UGONJWA UNAOTOKANA NA UTAPIAMLO

Washikadau katika sekta mbali mbali wametakiwa kushirikiana ili kuibali tatizo la utapia mlo miongoni mwa Watoto.

Kwa mujibu wa Richard Sijenyi ambaye ni afisa wa shirika lisilokuwa la kiserikali Compassionate National kuna haja ya taasisi muhimu katika jamii kama vile kanisa , shule na maafisa kwenye idara ya usalama hasa machifu na manaibu wao kuhamasishwa kuhusu madhara ya utapia mlo

.Afisa huyo ambaye amezungumza mjini Kisumu wakati wa hafla iliyowaleta Pamoja washikadau kutoka kaunti za Kisumu ,nandi na vihiga amelitaja tatizo hilo kuwa changamoto inayoadhiri afya ya Watoto hasa katika kaunti hizo tatu hali ambayo amehusisha na ukosefu wa maarifa.

Imetayarishwa na: Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *