WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI BARABARA YA MARSABIT-MOYALE

Watu wanne wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali ya barabarani eneo la Gof Chopa barabara ya Marsabit-Moyale.
Basi hilo lilikuwa likitoka Nairobi kuelekea Moyale kupitia Marsabit ajali hiyo ilipotokea.
Majeruhi wanapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Marsabit huku miili ya marehemu ikihifathiwa katika chumba cha maiti cha kituo hicho.
Imetayarishwa na Janice Marete