#Local News

KENYA KUANDAA PARA VOLLEY

Kenya iko tayari kuandaa Mashindano ya Para Volley Africa 2025 yanayoanza Jumamosi hii katika uwanja wa ndani wa Kasarani, huku zaidi ya nchi 10 zikitarajiwa kushiriki.

Kwa mara ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni, timu ya wanaume ya Kenya itapata fursa adimu ya kufukuzia ubingwa wa bara katika ardhi ya nyumbani, na Kocha Mkuu Julius Juma ana matumaini.

Ikihamasishwa na timu ya wanawake, ambayo ilimaliza ya pili nyuma ya Rwanda kwenye Mashindano ya Mpira wa Wavu ya afrika ya 2024 huko Lagos, timu ya wanaume inayoongozwa na nahodha Henry Caleb imeazimia kufanya makubwa.

Mashindano hayo yanatoa tiketi ya kucheza hatua ya kimataifa, kwani timu mbili bora zitafuzu kwa Mashindano ya Dunia ya Para Volley ya 2025 yaliyopangwa kufanyika Oktoba nchini Marekani.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KENYA KUANDAA PARA VOLLEY

MBOYA AJIVUNIA KUSHINDA TAJI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *