#Local News

OMTATAH MAHAKAMNI KUPINGA MSWADA WA KIFEDHA

Seneta wa Busia Okiya Omtatah na Mkenya mwingine kwa jina Dr. Benjamin Magare, wameelekea mahakamani kupinga vikao vinavyoendelea vya kukusanya maoni kuhusu mswada wa kifedha wa mwaka 2024-25, akisema mswada huo umewasilishwa mapema kabla ya bunge kuidhinisha makadirio ya bajeti.

Wameitaka mahakama kuorodhesha ombi lao kama la dharura, wakisema ni mahakama pekee inaweza kutoa suluhu.

Aidha, wanasema kwamba hatua hiyo ya bunge inakiuka vipengee vya sheria inayohusu matumizi ya fedha za umma.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

MZOZO WA UONGOZI WAENDELEA CHUONI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *