KLABU YA FORTUNE SACCO YASHINDWA KUPANDA DARAJA
KLABU ya Ligi ya Kitaifa daraja la pili, Fortune Sacco, italazimika kujaribu kupigania msimu mwingine katika harakati za kupanda Ligi Kuu, baada ya timu hiyo yenye maskani yake Kirinyaga kumaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wikendi iliyopita, nje kidogo ya safu ya mchujo kwa pointi nne pekee.
Licha ya kukatishwa tamaa, kocha mkuu Sylvestre Odero bado ana matumaini na kujivunia maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wake.
Odero, mwalimu kitaaluma, anasema wakati timu inapoelekea kwa matayarisho ya msimu ujao , watajipanga upya.
Nairobi United na APS Bomet, zilipandishwa daraja moja kwa moja hadi Ligi Kuu ya msimu ujao huku SS Assad na Muhoroni Youth zikishushwa daraja hadi FKF Division One.
Imetayrishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































