HATMA YA ‘WANYAKUZI’ WA ARDHI, MAAFISA

Watu 8 wakiwemo maafisa wawili wa wixzara ya ardhi wanaotuhumiwa na kuongoza misururu ya unyakuzi wa ardhi watasalia korokoroni kwa siku 4 zaidi ili kuiwezesha idara ya DCI kukamilisha uchunguzi dhidi yao.
Akitoa uamuzi huo, hakimu Robinson Ondieki amesema kuwa iwapo uchunguzi huo hautakamilika ndani ya siku hizo, wataachiwa huru kwa dhamana ya shilingi elfu 50 kila mmoja.
Aidha, watafika mahakamani tarehe 8 mwezi ujao kutajwa kwa kesi hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa