#Sports

STARLETS WANG’AA DHIDI YA BURUNDI

Vipusa wa timu ya taifa ya wanawake Harambee Starlets waliweka kando masaibu yao na kuwacharaza Burundi kwa mabao 3 bila jibu kwenye mechi yao ya ufunguzi katika mashindano yanayoendelea ya CECAFA Senior Women Challenge nchini Tanzania jana jioni.

Martha Amunyolet iliikabidhi Kenya hatamu za uongozi baada ya dakika 2, mshambuliaji huyo wa Vihiga Queens akionyesha weledi wake kwa kujipenyeza katikati ya mabeki wawili kabla ya kumkosesha faida mlinda lango wa Burundi Faida Habimana.

Ndani ya dakika 5 za mchezo, Starlets walikuwa na mabao mawili kimiani, Amunyolet kwa mara nyingine akifanya safi kwa kuiongoza pasi kutoka kwa Violet Nasaka, kabla ya Faith Mboya kuifungia bao la 3 katika muda wa majeruhi.

Kenya inashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2019 walipoicharaza Tanzania mabao 2 bila jibu kubeba taji hilo.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

STARLETS WANG’AA DHIDI YA BURUNDI

POLICE FC WATWAA TAJI LA KWANZA LA

STARLETS WANG’AA DHIDI YA BURUNDI

WAKENYA WATIA FORA DIAMOND LEAGUE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *