MAHAKAMA YATAKIWA KUMWAJIBISHA LANG’AT
Huku wakuu wa idara ya usalama wakiendelea kulaumiana kuhusiana na mauaji ya kusikitisha ya bloga Albert Ojwang, kundi la wanaharakati limewasilisha ombi mahakamani likitaka kuanzisha kesi ya kibinafsi dhidi ya naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lang’at kutokana na kifo hicho.
Kulingana na wanaharakati hao wakiongozwa na Julius Ogogo na Francis Auma, idara ya usalama na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma zimewafeli wakenya kwa kutomchukulia hatua Lang’at huku familia ya mwendazake ikihangaika.
Wakati uo huo, waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen amesema hatajiuzulu licha ya shinikizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































