GACHAGUA KIKAANGONI, MSWADA WA KUKOSA IMANI WAWASILISHWA

Seneta wa Tana River Danson Mungatana amewasilisha mswada katika bunge la seneti wa kutokuwa na imani na naibu rais Rigathi Gachagua kuhusiana na mienendo ya naibu huyo wa rais.
Akiwahutubia wanahabari, Mungatana amesema kwamba Gachagua amekiuka sheria inayodhibiti mienendo ya naibu rais na utekelezwaji wa majukumu yake.
Aidha, Mungatana amesema kuwa Gachagua amekuwa akitoa matamshi ya kibaguzi tangu aingie mamlakani, ikiwemo kuifananisha Kenya na kampuni ambako wenye hisa pekee ndio wanaofaa kunufaika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa