SI VIKAO VYA TIKTOK, KINGI AONYA MASENETA
Huku vikao vya kusikiliza hoja ya kumtimua kutoka mamlakani naibu rais Rigathi Gachagua vikiendelea kwa siku ya pili na mabayo inatarajiwa kuwa ya mwisho hii leo, spika wa bunge la senati Amason Kingi amewataka maseneta kuchukulia vikao hivyo kwa uzito.
Akitoa onyo ya kuwatimua baadhi ya maseneta, Spika Kingi amesema hoja hiyo ni suala zito kwa taifa na hivyo kanuni za seneti zinapaswa kuzingatiwa kwenye mchakato huo.
Onyo ya Spika Kingi imejiri kufuatia minong’ono kutoka kwa maseneta baada yao kupewa fursa ya kuwauliza mashahidi maswali kutoka tume ya EACC.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































