#Local News

SINA HAJA NA USHINDI WA 2027,ASEMA RAIS

Rais William Ruto anasema lengo lake kwa sasa sio kutwaa uongozi kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2027 bali kubadilisha taifa.

Akiongea huko Kajiado rais amekanusha madai kuwa serikali yake imekosa kutimiza ahadi nyingi ilizotoa kwa wakenya wakati wa kampeni.

Rais amekiri kuwa safari ya kuafikia mabadiliko anayolenga haijakuwa rahisi japo akaelezea kujitolewa kwake kuhakikisha ametimiza.

Amefichua kuwa kuna baadhi ya washauri waliomtaka kutotekeleza mengi katika muhula wake wa kwanza.

Imetayrishwa na Maureen Mukhobe

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *