WAKULIMA WA KAHAWA SIRISIA KUPATA HAKI, SERIKALI
Huenda wakulima wa kahawa walio chini ya chama cha ushirika cha Kikai eneo bunge la Sirisia kaunti ya Bungoma wakapata haki baada ya serikali ya kaunti hiyo kuanzisha ukaguzi wa vitabu vya hesabu kubaini iwapo kulikuwa na ufujaji wa fedha, siku moja baada ya wakurugenzi wa chama hicho kutimuliwa kutoka afisini.
Kwa mujibu wa afisa wa vyama vya ushirika Davis Nganga ambaye amezungumza baada ya uchaguzi wa wakurugenzi wapya, wakurugenzi waliotimuliwa watafunguliwa mashtaka iwapo ufujaji utabainika.
Wakati uo huo, wakulima wamehimiza ushirikiano kwenye chama hicho ili kuhakikisha uboreshaji wa maisha yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































