#Local News

MSHUKIWA ADAIWA KUWAUMA POLISI BUNGOMA

Polisi katika kaunti ya Bungoma wanatarajia kumfikisha mahakamani mshukiwa mmoja anayedaiwa kuwauma na kuwajeruhi maafisa 2 wa polisi kutoka kituo cha Namwela, waliokuwa wamekwenda kumkamata kwa tuhuma za uhalifu.

Kulingana na wakazi, maafisa 2 kati ya 3 waliokuwa wamefika nyumbani kwa jamaa huyo katika kijiji cha Sitabicha, walishambuliwa na mshukiwa aliyewauma begani na mikononi, ila afisa wa 3 akafanikiwa kumdhibiti.

Kamanda wa polisi Magharibi mwa nchi Issa Mohamud, amesema mshukiwa atafunguliwa mashtaka ya uharibifu wa mali kimaksudi, kuzuia kukamatwa na kuwashambulia polisi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MSHUKIWA ADAIWA KUWAUMA POLISI BUNGOMA

RUTO AWAPA MAGAVANA JUKUMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *