GACHAGUA ASIMULIA TUMAINI JIPYA
Naibu rais Rigathi Gachagua amedokeza kuwa viongozi kutoka eneo la mlima Kenya wanaounga azma yake ya kuwaunganisha viongozi wote wa eneo hilo huenda wakafanya maamuzi tofauti kwenye uchaguzi ujao wa mwaka wa 2027.
Akiwahutubia wafanyibiashara katika soko la Markiti jijini Nairobi mapema leo, Gachagua amesema mara hii wameweka mpangilio wa kuhakikisha wanahamasisha wakazi kupiga kura kwa makini kwa lengo kuu la kuendeleza maendeleo katika ukanda wa Mlima Kenya.
Gachagua amewatembelea wafanyibishara kwenye soko hilo wakati ambapo wanakabiliwa na tishio la kutimuliwa kutoka pale sokoni na kuelekezwa maeneo ya Eastlands. Amewahimiza viongozi wenzake kuwapa heshima wananchi hasaa wafanyabiashara.
Gachagua ameandamana na wabunge na wawakilishi wadi kadhaa wanaomuunga mkono.
Imetayarishwa na Kennedy Osoro
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































