#Local News

ALIYEKUWA MBUNGE WA EMBU ANASAKWA NA POLISI

Maafisa wa upelelezi wanamsaka aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Kaunti ya Embu baada ya kuhusika katika kisa cha ufyatulianaji risasi katika Mji wa Embu jana Jumapili.

Kwa mujibu wa mbunge huyo wa zamani ni mmiliki wa bunduki aliye na leseni.

Inasemekana alikuwa na ugomvi na mtu aliyekuwa akifurahiya katika eneo moja la burudani mjini humo na kusababisha kufyatuliana risasi.

Polisi wanasema hakuna mtu aliyejeruhiwa kutokana na kupigwa risasi lakini baadhi ya watu waliokuwa wakisherehekea walipata michubuko walipokuwa wakitoroka kutafuta usalama wao.

Juhudi za kumtafuta mbunge huyo wa zamani zingali zinaendelea huku polisi wakimshauri ajisalimishe.

Imetayarishwa na Janice Marete

ALIYEKUWA MBUNGE WA EMBU ANASAKWA NA POLISI

SENETA ONYONKA; NAJUA NINACHOKISEMA

ALIYEKUWA MBUNGE WA EMBU ANASAKWA NA POLISI

RAILA AWASILISHA RASMI AZMA YA AUC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *