WATOTO WATATU WAANGUSHWA NA GARI LA POLISI KITUI
Watoto watatu wenye umri wa kati ya miaka saba na minane wanapokea matibabu katika hospitali moja huko Kyuso, Kaunti ya Kitui baada ya kuangushwa na gari la polisi jana jumapili.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kamuwongo huku polisi wakiendesha gari kutoka Kakunike kuelekea Kyuso.
Kwa mujibu wa Chifu msaidizi wa eneo hilo David Mwendwa watoto hao walikuwa wakielekea nyumbani baada ya kuhudhuria ibada kanisani.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































