MARAGA ATAKA KENYA KWANZA ING’OKE
Hisia mbali mbali zimeendelea kuibuka kufuatia kifo cha bloga Albert Ojwang, aliyekuwa jaji mkuu David Maraga akitaka Rais William Ruto kusitisha utawala wake mara moja na kuondoka mamlakani na serikali yake kwa kushindwa kuwalinda wakenya.
Kupitia taarifa, Maraga amerejelea ripioti ya upasuaji wa mwili wa Ojwang, mauaji ya zaidi ya wakenya 100 na utekaji nyara wakati wa maandamano ya kizazi cha Gen Z mwaka jana.
Aidha, ametaja kifo cha Ojwang kama sababu ya mwisho ya wakenya kuchoshwa na utawala huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































