MADAKTARI, WAUGUZI WATISHIA MGOMO WA KITAIFA

Huenda wakenya wanaosaka huduma za kimatibabu katika hospitali za umma wakajipata kwenye hali ngumu kwa mara nyingine tena, baada ya muungano wa madaktari KMPDU kutoa makataa ya siku 14 kwa serikali iwalipe malimbikizi ya mishahara yao la sivyo wagome.
Katika kikao na wanahbari, katibu mkuu wa KMPDU Davji Atellah ameonyesha masikitiko kuhusiana na kucheleweshwa kwa malipo yao, akisema hatua hiyo imewasababishia mahangaiko madaktari kote nchini.
Wakati uo huo, katibu mkuu wa muungano wa wauguzi Seth Panyako, ameunga mkono mgomo huo, akizitaka serikali za kaunti kuangazia changamoto hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa