#Local News

PIGO KWA CHAMA CHA KANU BAADA YA MAHAKAMA KUINYIMA UMILIKI WA KICC

Mahakama Kuu imetoa uamuzi kuwa jumba la mikutano la  Kimataifa la (KICC) ni la Serikali ya Kenya, na kutupilia mbali ombi la chama cha Kenya African National Union (KANU) kilichotaka kutangazwa kama mmiliki wa jumba hilo

Katika uamuzi wake  Jaji Jackline Mogenyi amesema kuwa kamishna wa ardhi mnamo 1989 hakuwa na uwezo wa kutenga ardhi hiyo kwa KANU

Kwa miaka mingi, KANU imekuwa ikidai umiliki wa mali hiyo, na imeiorodhesha miongoni mwa mali zake kwenye faili kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa.

KICC ilidhaniwa kuwa mali ya KANU hadi pale serikali ya marehemu aliyekuwa rais wa tatu Emilio Mwai Kibaki ilipoichukua mwaka wa 2003.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *