MENEJA WA NGCDF MASHAKANI

Mahakama imewapa walalamishi watatu kibali cha kuwasilisha malalamishi yao dhidi ya meneja wa Hazina ya Maendeleo ya Eneo bunge la Kiambaa Lorna Muthoni Njoroge mbele ya bodi ya NGCDF katika muda wa siku saba.
Jaji Byram Ongaya amewaagiza walalamishi hao kuwa iwapo watashindwa kufanya hivyo basi kesi hiyo itafutiliwa mbali bila amri ya gharama.
Katika kesi hiyo Richard Mulwa Musyoka, Richard Nzine, Nicholas Michael na Elizabeth Mumbi waliiomba waliwasilisha kesi mahakamani wakimtaka meneja huyo wa NGCDF Lorna Muthoni Njoroge aondolewa afisini kwa madai kwamba hafai kuhudumu.
Imetayarishwa na Janice Marete