UASU WATISHIA KUGOMA
Muungano wa wafanyikazi wa vyuo vikuu umetoa notisi ya siku saba ya mgomo kulalamikia kucheleweshwa na kutolipwa mishahara yao yote.
Katibu mkuu wa UASU Constantin Wesonga ametangaza kuwa notisi hiyo itaanza kutumika mara moja na kutishia kulemaza masomo katika vyuo vikuu vyote vya umma wakati ambapo wanafunzi wapya na wanaoendelea watakaporipoti shuleni.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































