#Local News

MAAFISA 11 WA KAUNTI YA VIHIGA WAKAMATWA KWA WIZI WA MILIONI 17

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi imewakamata maafisa 11 katika Serikali ya Kaunti ya Vihiga huku ikianzisha uchunguzi kuhusu tuhuma za wizi wa Shilingi milioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuongeza damu.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari tume hiyo waliokamatwa ni pamoja na Afisa Mkuu wa Huduma za Matibabu Dkt Arnold Kimiyia Mamadi na Mkurugenzi wa Ununuzi Godfrey Oyaro.

Ni miongoni mwa washukiwa 11 wanaotarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kupambana na Ufisadi ya Kakamega hii leo.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *