#Local News

SHOKA LA KK, FURAHA YA ODM

Katika kile kinachoonekana kama kuwaadhibu wandani wa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, mrengo wa Kenya Kwanza umewatimua kutoka uongozi wa kamati mbali mbali katika bunge la kitaifa, chama cha ODM kikiratibiwa kunufaika pakubwa na uongozi wa kamati hizo.

Kwenye mageuzi hayo, mbunge wa Embakasi North James Gakuya ameondolewa kutoka uwenyekiti wa kamati ya biashara, Gathoni Wamuchomba wa Githunguri akiondolewa kutoka uwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa katiba na kuwa tu mwanachama, sawa na Ndindi Nyoro wa Kiharu ambaye amepokonywa uwenyekiti wa kamati ya bajeti na kufanywa kuwa mwanachama.

Mbunge wa Alego Usonga Sam Atandi na mwenzake wa Ikolomani Benard Shinali wameratibiwa kuongoza kamati za bajeti na biashara mtawalia.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *