‘ALIYEMJERUHI’ POLISI AKAMATWA BONDO

Makachero wa idara ya upelelezi DCI wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kumshambulia afisa wa polisi wakati wa maaandamano ya kupinga mswada wa fedha katika eneo la Bondo kaunti ya Siaya
Kulingana na DCI, mshukiwa huyo ambaye ametambuliwa kama Sostine Otieno alikuwa miongoni mwa wahalifu waliovamia kituo cha polisi cha Bondo wakiwa wamejihami na silaha butu ikiwa mawe na manati.
DCi imesema washukiwa waliwajeruhi vibaya maafisa kadhaa wa polisi, mmoja wao akiwa amelazwa katika hospitali ya Bondo akiwa katika hali mahuti, na kuharibu mali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa