UASU YASISITIZA MGOMO UNGALIPO

Shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma zimeendelea kuathirika kwa siku ya pili sasa kufuatia mgomo wa wahadhiri, ambao wamesisitiza kwamba hawatarejea kazini hadi makubaliano yao n aserikali yaliyowafanya kurejea kazini yatakapotekelezwa.
Kupitia kwa muungano wao wa UASU, wahadhiri wameitaka serikali kuwajibika na kutekeleza makubaliano hayo, waliyotia Saini na wizara ya leba kabla ya kumaliza mgomo uliodumu kwa takribani wiki mbili.
Miongoni mwa makubaliano hayo ni nyongeza ya kati ya asilimia 7-10 kwa mishahara ya wahadhiri.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa